25 Oct Hambaga ya Kukaanga
MUDA UTAKAOTUMIKA KWA UJUMLA
Saa 2
UGUMU
KWA
Watu 4
VIAMBATO
- 250g za unga
- 150ml za maji ya vuguvugu
- Kijiko kidogo 1 cha chumvi
- 5 1/2g za hamira ya Saf-Instant
- 30g za siagi laini
- 150g za nyama ya kusaga iliyoundwa kama bapa la mviringo x 4
- Nyanya 1 iliyosagwa
- Nyanya 1 iliyokatwa slesi
- Slesi nne za vipande vya jibini laini
- Majani manne ya saladi
- Kijiko kikubwa 1 cha kitimiri
- Kitunguu 1 kilichosagwa
- Vipande 3 vya kitungu saumu
- Kijiko kidogo 1 cha pilipili manga
- Kijiko kidogo 1 cha unga wa nyanya
- Mafuta ya kukaangia
BIDHAA INAYOANGAZIWA
1
Weka unga, chumvi, unga wa nyanya na hamira ya Saf-Instant kwenye bakuli kisha changanya.
2
Tengeneza tundu katikati, ongeza maji na siagi laini alafu kanda na unda manda iwe kama mpira.
3
Funika na acha itulie kwa muda wa saa 1.
4
Toa hewa kwenye manda, kanda alafu gawa kwenye vipande vinne na viunde viwe mviringo.
5
Kandamiza kila mviringo kisha acha viumuke kwa muda wa saa 1.
6
Kaanga kwa muda wa dakika 3 hadi 4 kwenye mafuta ya moto wa wastani, kisha toa ukaushe kwenye karatasi ya kunyonya mafuta.
7
Kwa vijazio: Katika kikaangio weka mafuta, vibapa vya nyama, chumvi, pilipili manga, kitunguu, nyanya ya kusagwa, kitunguu saumu na kitimiri. Changanya na pika kwa muda wa dakika 5.
8
Yayusha vipande vya jibini.
9
Pangilia hambaga.
You may also like:
Sorry, the comment form is closed at this time.