flap saf-instant

Let’s
make it
happen!

SAF-INSTANT-11g-RED

Na Saf-instant®, tunakuletea hamira fanisi sana, iliyorahisi kutumia na ambayo itakupa matokeo yanayolingana na mategemeo yako kila wakati, ili uwapatie wale unaowajali kile kilicho bora kabisa.

Saf-instant®, hamira kavu ya papo hapo ya kuokea, inayorahisisha maisha kwa wale wanaopenda kutengeneza mikate yayo wenyewe!

Easy-to-use-107x107

RAHISI KUTUMIA

Hamira kavu ya Saf-instant® haihitaji kuchanganywa kwanza kwenye maji, unaweza kuiongeza moja kwa moja kwenye unga wako kabla ya kukanda.

Package-107x107

VIPIMO VYA VIFURUSHI VINAVYOFAA

Vipimo anuwai vinavyofaa kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na kwa aina zote za mapishi.

URAHISI WA KUHIFADHI

Hakuna haja ya kuhifadhi Saf-instant® kwenye baridi

Our tips with Saf-instant® yeast

Msimamo wa Saf-instant® ni kusaidia waokaji wa nyumbani siku hadi siku kwa kufanya kila kiwezekanacho kutimiza mategemeo yao. Hapa tunajibu maswali yaulizwayo mara kwa mara.

Mambo ya msingi juu ya hamira

Je, hamira inaathari vipi ladha ya mkate?

Usitawishaji wa ladha na harufu nzuri ya mkate hufanyika wakati wa mchakato wa uokaji, haswa wakati wa hatua za kuumuka na kuoka na kwa kiasi kidogo zaidi wakati wa kukanda.

Hamira inawezesha harufu nzuri maalum kusitawi (zaidi ya molekuli 540 za harufu nzuri zimetambuliwa) kulingana na hali ya kuoka (viambato na mchakato). Hivyo huupa mkate vitambulishi vyake binafsi vya harufu nzuri. Hamira pia hufanya kazi muhimu kwenye rangi na umbile asili la gamba la mkate.

Je, tofauti kati ya hamira ya kuokea na hamira magadi ni nini?

Hamira ya kuokea ni bidhaa iliyo hai na tendaji, ni kuvu isiyoweza kuonekana bila hadubini ambayo inawezesha manda kuumuka (kwa kutengeneza gesi), ili kutengeneza harufi nzuri. Hamira ya kuokea huwezesha kupata bidhaa za mkate: mkate, vitobosha na manda za pizza.

Hamira magadi inatengenezwa na magadi, tatariki ya haidrojeni ya potasiamu na wanga wa mahindi na haiwezeshi kuumuka, hivyo haiwezeshi kuoka mkate. Inatumika kutengeneza keki.

Kama unataka kuoka mkate nyumbani, utahitaji kutumia hamira ya kuokea.

Je, tofauti kati ya hamira mbichi na hamira kavu ni nini?

Hamira mbichi bado ina maji ndani yake. Hii huwa ni kipande cha malhamu au tonge laini la rangi nyeupe au ya mchanga, inayomeng’enyeka kiurahisi. Inaweza kuhifahifadhiwa kwenye friji (jokofu) kati ya mionzi ya C 0° na 4°.

Hamira kavu ni hamira ambayo imetolewa maji na ambayo inafanana na chembechembe au tambi nyembamba. Hamira hii, kwa kawaida inauzwa kwenye vipaketi vya gramu 11, inaweza kuhifadhiwa kwa muda wa miaka miwili kwenye halijoto ya kawaida na katika sehemu kavu.

Je, tofauti kati ya hamira kavu tendaji na hamira kavu ya papo hapo ni nini?

Hamira kavu tendaji ni vijichembechembe au vijitufe vidogo. Hamira hubainishwa na uthabiti wake mzuri na huhifadhika vizuri katika mazingira magumu. Lazima kwanza iyayushwe kwenye maji au maziwa kidogo ya uguvugu.

Hamira kavu ya papo hapo kama Saf-instant® huwa ni vijitambi vidogo ambavyo vinaweza kujumuishwa kiurahisi kwenye manda. Ili kudumisha ufanisi wake, hamira kavu za papo hapo huwekwa kwenye vifurushi vya ombwe (vilivyonyonywa hewa yote) au vya mazingira yanayohifadhi. Lazima vihifadhiwe kwenye hali kavu na halijoto ya kawaida.

Je, hamira Saf-instant® ni asilia?

Hamira ni kiumbehai, kipatikanacho kiasilia duniani. Kuna aina tofauti za hamira mwituni na mbegu ya Saccharomyces cerevisiae imechaguliwa kwa ajili ya utengenezaji mikate. Spishi hii ya hamira ilitolewa mwituni na kufugwa ili kuifanya ipatikane kwa waokaji wote. 

Je, hamira ni nzuri kwa afya yako?

Hamira zina lishe nyingi sana na zinaweza kuongeza athari ya kiutendaji ya vyakula kwa namna ya kiasilia. Kwa kuwa ina madini, vitamini na asidi za amino, hamira ina manufaa mengi. Kwa msaada wa vitu hivi ambavyo ni vya muhimu kabisa kwa afya nzuri ya mwili wa binadamu, hamira hufanya kazi ya kilishe katika lishe yetu na usawa wa miili yetu. Kwa mfano, hamira na vitokanavyo vyake hutumika katika visaidizi vya chakula ili kuleta nyongeza kwenye lishe yetu, kuwezesha usitawi wetu na kuchangia uboreshaji wa afya yetu.

Je, E491 inayotumika katika utengenezaji wa hamira ni nini?

E491 ni kilanishaji chenye asili ya kimimea tu (sorbitani monostearate), ambacho kazi yake ni kulinda seli za hamira wakati wa mchakato wa kuikausha.

Je, hamira ya Saf-instant® inaweza ikaidhinishwa kuwa halali?

Hamira ya Saf-instant® inaidhinishwa kuwa ni halali. 

Je hamira ya kuokea hutumika namna gani?

Je, hamira inatumiwaje kiusahihi?

Saf-instant® ni rahisi sana kutumia! Unaweza kuiongeza moja kwa moja kwenye viambato vikavu kabla ya kuchanganya ila epusha kuiweka moja kwa moja kwenye chumvi.

Kama unatumia mashine ya kutengeneza mikate, kwanza mimina viambato vyote vya mapishi yako kasoro unga na hamira, kisha ongeza unga alafu hamira.

Je, ninahitaji kuchanganya hamira na maji kabla ya kuitumia?

Inategemeana na aina ya hamira. Sio lazima kuchangana hamira kavu ya papo hapo na maji kama ifanywavyo kwa Saf-instant®, ila unaweza kuichanganya na maji kidogo ili kupata mchanganyiko unaolingana zaidi.

Je, ninahifadhi vipi hamira?

Hamira ya kuokea ni bidhaa hai na isiyostahamili mionzi ya joto iliyojuu. Ili iwe fanisi vizuri, lazima ihifadhiwe katika hali nzuri kabisa. Ni muhimu kuiepusha ikutane na hewa.

Hamira kavu kama Saf-instant iliyowekwa kwenye vifurushi ombwe au kwenye mazingira yanayohifadhi, inapaswa ihifadhiwe katika sehemu iliyokavu na ya halijoto ya kawaida. Hivyo itakaa ikiendelea kuwa fanisi. Unaweza kuiwekea utepe wa gundi ili kuepusha hewa kuingia. Kuhifadhi kwenye ubaridi kunaweza kusaidia kuongeza muda wa ufanisi wa hamira.

Je, ninaweza kugandisha kwenye barafu hamira?

Hamira inaweza kugandishwa kwenye barafu.  Hamira kavu ya papo hapo huganduka haraka sana na huendelea kuwa na ulaini wake wote. Hivyo inaweza kuongezwa moja kwa moja kwenye unga wako.

Je, unaweza kuhifadhi hamira ya Saf-instant® muda gani baada ya kuifungua?

Saf-instant® lazima ihifadhiwe katika sehemu kavu mbali na joto. Ikishafunguliwa, paketi lazima itumike ndani ya saa 48 au ihifadhiwe kwenye friji, ikiwa imefugwa na itumike ndani ya siku 8.