25 Oct Mafini ya Mkate Mtamu yenye Chokoleti na Karanga
MUDA UTAKAOTUMIKA KWA UJUMLA
Saa 2
UGUMU
KWA
Watu 6
1
Weka unga, chumvi, sukari, karanga na hamira kwenye bakuli kisha vichanganye vikiwa vikavu.
2
Ongeza mayai, maziwa, siagi alafu changanya vyote.
3
Kanda mpaka manda iache kuganda mikononi. Unda iwe mviringo kama mpira, funika na iache iumuke kwa muda wa saa 1.
4
Toa hewa kwenye manda na ikate vipande 6.
5
Viunde viwe kama mpira kisha viweke kwenye chombo cha kuokea mafini.
6
Funika na viache viumuke kwa muda wa dakika 30.
7
Vipange kwenye chombo kikubwa zaidi ukiacha nafasi ya kutosha kati ya kila moja, paka yai lililopigwa juu alafu nyunyizia vipande vya chokoleti.
8
Oka kwenye oveni yenye joto la 180oC kwa muda wa 20 min.
You may also like:
Sorry, the comment form is closed at this time.