14 Mar Mkate wa Fokachia wa Hamu na Jibini
MUDA UTAKAOTUMIKA KWA UJUMLA
Saa 4 30
UGUMU
KWA
6
VIAMBATO
- 5.5g hamira ya Saf-instant Dry Yeast
- 1 kijiko kidogo vya chumvi
- 1 kijiko kikubwa cha tangawizi kavu iliyosagwa
- 1 kijiko kidogo cha pilipili manga
- 1 kijiko kikubwa cha sukari nyeupe
- 3 vijiko vikubwa vya tomato sosi
- 250g unga
- 150g hamu ya nyama ya ng’ombe
- 150g jibini ya mozarela
- 1 nyanya
- 150ml maji ya vuguvugu
- 50ml mafuta ya alizeti
BIDHAA INAYOANGAZIWA
1
Changanya unga, sukari, tangawizi kavu iliyosagwa, chumvi, pilipili manga, hamira kavu ya Saf-instant Dry Yeast alafu koroga.
2
Changanya pamoja maji na mafuta mpaka vichanganyike vizuri.
3
Kanda kwa muda wa dakika 20.
4
Weka manda ndani ya bakuli.
5
Funika na kisha acha iumuke kwa muda wa saa 2 kwenye friji.
6
Hamishia kwenye chombo kipana cha mviringo cha kuokea kilichopakwa mafuta.
7
Sambaza manda iwe tambarare
8
Funika na kisha acha iumuke kwa muda wa dakika 2.
9
Ongeza tomato sosi na weka matundu kwa kutumia vidole vyako.
10
Weka jibini, hamu na nyanya.
11
Oka kwenye oveni ya 180o kwa dakika 20.
Furahia!
You may also like:
Sorry, the comment form is closed at this time.