27 Sep Mkate wa karanga
MUDA UTAKAOTUMIKA KWA UJUMLA
Saa 2
UGUMU
KWA
Watu 6
1
Weka unga, chumvi, sukari na hamira kwenye bakuli kisha vichanganye vikiwa vikavu.
2
Ongeza yai, siagi na maji kisha changanya alafu kanda mpaka manda iache kuganda mikononi.
3
Changanyia humo karanga na endelea kukanda manda.
4
Unda manda iwe kama mpira na acha itulie kwenye bakuli kwa muda wa dakika 10.
5
Toa hewa kwenye manda na igawanye kwenye vipande vidogo vidogo, viunde vizuri kisha viweke kwenye sinia la oveni. Acha viumuke kwa muda wa saa 1 na dakika 30.
6
Chanja vipande kwa kutumia wembe.
7
Oka kwenye oveni yenye joto la 200oC kwa muda wa 15 min.
You may also like:
Sorry, the comment form is closed at this time.