Mkate wa kukaanga kwa kuku

Mkate wa kukaanga kwa kuku

preparation-75x75

MUDA UTAKAOTUMIKA KWA UJUMLA

Saa 2h30

difficulty-75x75

UGUMU

medium
portions-75x75

KWA

Watu 4

Whisk

VIAMBATO

 • 5.5g za hamira ya Saf-Instant
 • 425g za unga
 • 1 kijiko kidogo cha chumvi
 • 2 kijiko kidogo cha sukari ya kahawia
 • 250 ml za maji ya vuguvugu
 • 1/2 kijiko kidogo cha iliki
 • 2 vijiko vikubwa vya mafuta
 • 1 kijiko kidogo cha pilipili manga
 • 1 kijiko kidogo cha tangawizi iliyosagwa
 • Chumvi kidogo
 • 1 karoti
 • 1 kitunguu chekundu
 • 1 pilipili hoho
 • 250 g za minofu ya kuku
 • 3 vipande vya kitunguu saumu

BIDHAA INAYOANGAZIWA

1

Weka unga, chumvi, sukari, iliki na hamira ya Saf-Instant kwenye bakuli kisha vichanganye na tengeneza tundu katikati.

2

Mimina maji ya vuguvugu kwenye tundu kisha kanda manda mpaka ichanganyike vizuri.

3

Funika na kitambaa kisafi kisha acha iumuke kwenye sehemu yenye joto la wastani kwa muda wa saa 1.

4

Kanda manda tena mpaka iwe imara zaidi. Sukuma manda mpaka iwe na unene wa 2 cm kisha kata miviringo kadhaa. Acha iumuke kwa muda wa saa 1.

5

Kaanga miviringo kwenye mafuta mengi mpaka igeuke rangi ya kahawia isiyokolea sana. Baada ya kuiva, itoe kwenye mafuta na iweke kwenye karatasi ya jikoni iyonye mafuta.

6

Acha ipoe kisha kata kila kipande katikati ili kuweka vijazio vya kuku.

7

Weka mafuta kwenye sufuria na kaanga kitunguu na vitunguu saumu vilivyo katwa katwa. Ongeza minofu ya nyama ya kuku na tangawizi iliyosagwa.

8

Weka, chumvi na pilipili manga kisha pika kwa muda wa dakika 5. Ongeza pilipili hoho na karoti kisha endelea kupika kwa muda wa dakika 5 zaidi.

9

Jazia kijazio cha nyama ya kuku.

10

Huu Tayari!

Unaweza pia kupenda:

No Comments

Sorry, the comment form is closed at this time.